Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 64


Sehemu ya 64

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa wazee wa Kanisa, huko Kirtland, Ohio, 11 Septemba 1831. Nabii alikuwa akijiandaa kwenda Hiram, Ohio, kuanza tena kazi yake ya kutafsiri Biblia, ambayo iliwekwa pembeni wakati alipokuwa Missouri. Kikundi cha ndugu ambao walikuwa wameamriwa kusafiri kwenda Sayuni (Missouri) walikuwa wamejishughulisha katika kufanya maandalizi ya kuhama mwezi wa Oktoba. Katika wakati huu wa shughuli nyingi, ufunuo huu ulipokelewa.

1–11, Watakatifu wanaamriwa kusameheana, isije dhambi kubwa ikabaki kwao; 12–22, Wasiotubu wataletwa mbele ya Kanisa; 23–25, Yule ambaye amelipa zaka hataunguzwa wakati Bwana ajapo; 26–32, Watakatifu waonywa kuepuka madeni; 33–36, Waasi watatupwa nje ya Sayuni; 37–40, Kanisa litayahukumu mataifa; 41–43, Sayuni itastawi.

1 Tazama, hivyo ndivyo asemavyo Bwana Mungu wenu kwenu, Enyi wazee wa kanisa langu, sikilizeni na sikieni, na yapokeeni mapenzi yangu juu yenu.

2 Kwani amini ninawaambia, kuwa nataka kwamba amuushinde ulimwengu; kwa hiyo nitakuwa na bhuruma juu yenu.

3 Wapo watu miongoni mwenu ambao wametenda dhambi; lakini amini ninawaambia, kwa mara hii moja, kwa ajili ya autukufu wangu mwenyewe, na kwa ajili ya wokovu wa nafsi, bnimewasamehe dhambi zenu.

4 Nitakuwa mwenye huruma kwenu, kwani nimewapa ufalme.

5 Na afunguo za siri za ufalme hazitachukuliwa kutoka kwa mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, kwa njia niliyoteua, wakati akiwa hai, kadiri yeye atakavyotii bibada zangu.

6 Kuna wale ambao wametafuta kupata sababu za kumshtaki bila sababu;

7 Hata hivyo, yeye ametenda dhambi; lakini amini ninawaambia, Mimi, Bwana, ahusamehe dhambi kwa wale wenye bkuungama dhambi zao mbele zangu na kuomba msamaha, wale ambao hawakutenda dhambi ya cmauti.

8 Wanafunzi wangu, katika siku za kale, walitafuta amakosa kati yao na wala hawakusameheana katika mioyo yao; na kwa uovu huu walipata mateso na bkuadhibiwa vikali.

9 Kwa hiyo, ninawaambia, kwamba mnapaswa akusameheana ninyi kwa ninyi; kwani yule basiyemsamehe ndugu yake makosa yake husimama na hatia mbele za Bwana; kwa kuwa ndani yake imebaki dhambi kubwa.

10 Mimi, Bwana, anitamsamehe yule nitakaye kumsamehe, lakini ninyi mnatakiwa bkuwasamehe watu wote.

11 Nanyi mnapaswa kusema mioyoni mwenu—Mungu na aahukumu kati ya mimi na wewe, na akulipe sawasawa na bmatendo yako.

12 Na yule asiyetubu dhambi zake, na hazikiri, mtamleta mbele ya akanisa, na mtamfanya kama maandiko yanavyowaambia iwe kwa amri au kwa ufunuo.

13 Na hili mtalifanya ili Mungu aweze kutukuzwa—siyo kwa sababu ninyi hamsamehi, hamna huruma, bali kwamba ninyi msiwe na hatia machoni pa sheria, ili msimkosee yeye ambaye ni mtunga sheria wenu—

14 Amini ninasema, kwa sababu hii mtafanya mambo haya.

15 Tazama, Mimi, Bwana, nilikasirishwa na yule aliyekuwa mtumishi wangu Ezra Booth, na pia mtumishi wangu Isaac Morley, kwa kuwa hawakuishika sheria, wala amri;

16 Walitafuta ubaya katika mioyo yao, na Mimi, Bwana, nilimzuia Roho wangu. aWalishutumu kwa uovu jambo ambalo ndani yake hapakuwa na uovu; hata hivyo nimemsamehe mtumishi wangu Isaac Morley.

17 Na pia mtumishi wangu aEdward Partridge, tazama, ametenda dhambi, na bShetani anatafuta kuangamiza roho yake; lakini wakati mambo haya yatakapokuwa yamejulikana kwao, nao wakatubu uovu wao, watasamehewa.

18 Na sasa, amini ninasema kwamba ninaona ni muhimu kuwa mtumishi wangu Sidney Gilbert, baada ya wiki chache, arejee katika shughuli zake, na kwenye uwakala wake katika nchi ya Sayuni;

19 Na kile alichokiona na kusikia anaweza kuwajulisha wanafunzi wangu, ili wasiangamie. Na ni kwa sababu hii nimeyasema mambo haya.

20 Na tena, ninawaambia, kuwa mtumishi wangu Isaac Morley aasijaribiwe kupita awezavyo, na kutoa ushauri potofu utakaowaumiza, nilitoa amri kuwa shamba lake liuzwe.

21 Sitaki mtumishi wangu Frederick G. Williams auze shamba lake, kwani Mimi, Bwana, ninataka kupaimarisha mahali hapa katika nchi ya Kirtland, kwa kipindi cha miaka mitano, kipindi ambacho sitawaangusha waovu, ili kwamba kwa njia hii niweze kuwakomboa baadhi yao.

22 Na baada ya siku hiyo, Mimi, Bwana, sitamshika na ahatia yeyote ambaye atakwenda na moyo uliofunguka katika nchi ya Sayuni; kwa kuwa Mimi, Bwana, ninaitaka bmioyo ya wanadamu.

23 Tazama, sasa inaitwa aleo hadi bkuja kwa Mwana wa Mtu, na hakika ni siku ya ckujitoa dhabihu, na siku ya watu wangu kulipa zaka; kwani yule ambaye danalipa zaka ehataunguzwa moto wakati wa kuja kwake.

24 Kwani baada ya leo kwaja akuungua—hii nikiongea kwa jinsi ya Bwana—kwani amini ninasema, kesho wote wenye bkiburi na wote watendao uovu watakuwa makapi; na Mimi nitawachoma, kwani Mimi ndimi Bwana wa Majeshi; na sitamwacha yeyote ambaye atabaki katika cBabilonia.

25 Kwa hiyo, kama mnaniamini Mimi, mtafanya kazi wakati ingali inaitwa leo.

26 Na siyo vyema kwamba watumishi wangu aNewel K. Whitney na Sidney Gilbert, wauze bmaduka yao na mali zao hapa; kwa kuwa hiyo siyo hekima hadi mabaki ya kanisa, ambayo yamebakia mahali hapa, watakapokwenda katika nchi ya Sayuni.

27 Tazama, inasemekana katika sheria zangu, au umekatazwa, kujiingiza katika adeni kwa maadui zako;

28 Lakini tazama, haijasemwa wakati wowote kwamba Bwana hatachukua wakati atakao, na kulipa wakati aonavyo yeye kuwa ni vyema.

29 Kwa hiyo, ninyi mkiwa kama mawakala, mpo katika utumishi wa Bwana; na lolote mfanyalo sawasawa na mapenzi ya Bwana ni kazi ya Bwana.

30 Na amewaweka ninyi kuwahudumia watakatifu wake katika siku hizi za mwisho, ili waweze kujipatia aurithi katika nchi ya Sayuni.

31 Na tazama, Mimi, Bwana, ninawatangazia, na amaneno yangu ni hakika na hayatakuwa bbure, kwamba watapata.

32 Lakini mambo yote lazima yatakuja kutimia katika wakati wake.

33 Kwa hiyo, amsichoke kutenda mema, kwa kuwa mnaijenga misingi ya kazi kubwa. Na kutokana na bmambo madogo huja yale yaliyo makuu.

34 Tazama, Bwana aanahitaji bmoyo na akili yenye kukubali, na wenye kukubali na ckutii watakula mema ya Sayuni katika siku za mwisho.

35 Na awaasi bwatakatiliwa mbali kutoka nchi ya Sayuni, na watapelekwa mbali na hawatairithi nchi.

36 Kwani, amini ninawaambia, kwamba waasi siyo wa damu ya aEfraimu, kwa hiyo wataondoshwa.

37 Tazama, Mimi, Bwana, nimelifanya kanisa langu katika siku hizi za mwisho kuwa kama mwamuzi aliyekaa juu ya mlima, au katika mahali pa juu, kuwahukumu mataifa.

38 Kwani itakuwa kwamba wakazi wa Sayuni awatahukumu mambo yote yahusuyo Sayuni.

39 Na waongo na wanafiki watadhihirishwa na wao, na wale wasio amitume na manabii watajulikana.

40 Na hata aaskofu, ambaye ni bmwamuzi na washauri wake, ikiwa siyo waaminifu katika cusimamizi wao watahukumiwa, na dwengine watapandwa badala yao.

41 Kwani, tazama, ninawaambia ninyi kwamba aSayuni itastawi, na butukufu wa Bwana utakuwa juu yake;

42 Naye atakuwa abendera kwa watu, na hapo watakuja kutoka kila taifa chini ya mbingu.

43 Na siku itakuja ambayo mataifa ya dunia ayatatetemeka kwa sababu yake, na wataogopa kwa sababu ya wingi wao watishao. Bwana amesema hili. Amina.