Msaada wa Masomo
Sayuni
iliyopita inayofuata

Sayuni

Walio safi moyoni (M&M 97:21). Sayuni pia humaanisha mahali ambapo walio safi moyoni huishi. Mji uliojengwa na Henoko na watu wake ambao hatimaye ulitwaliwa mbinguni kwa sababu ya uadilifu uliitwa Sayuni (M&M 38:4; Musa 7:18–21, 69). Katika siku za mwisho mji uliopewa jina la Sayuni utajengwa karibu na Wilaya ya Jackson, Missouri (Marekani), ambako makabila ya Israeli yatakusanyika (M&M 103:11–22; 133:18). Watakatifu wanashauriwa kuijenga Sayuni mahali popote wanapoishi ulimwenguni.