Mamlaka na uwezo ambao Mungu humpa mwanadamu ili atende katika mambo yote kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu (M&M 50:26–27 ). Waumini wa Kanisa wanaume walio na ukuhani wametengwa katika akidi nao wamepewa mamlaka ya kufanya ibada na shughuli fulani za kiutawala katika Kanisa.
Wanaume huitwa kama makuhani wakuu kwa sababu ya imani na matendo yao mema yanayopita kiasi, Alma 13:1–12 .
Ninawapa ninyi uwezo wa kubatiza, 3Â Ne. 11:21 .
Ninyi mtakuwa na uwezo wa kutoa Roho Mtakatifu, Moro. 2:2 .
Nitaufunua kwenu ukuhani, kwa mkono wa Eliya, M&M 2:1 (JS—H 1:38 ).
Bwana alithibitisha ukuhani juu ya Haruni na kizazi chake, M&M 84:18 .
Ukuhani huu mkuu zaidi huhudumia injili, M&M 84:19 .
Alimchukua Musa kutoka katikati yao, na Ukuhani Mtakatifu pia, M&M 84:25 .
Kiapo na agano la ukuhani vinaelezwa, M&M 84:33–42 .
Ukuhani umedumu kupitia safu ya uzao wa baba zenu, M&M 86:8 .
Katika Kanisa kuna kuhani mbili, M&M 107:1 .
Ukuhani wa kwanza ni Ukuhani Mtakatifu, kwa Mfano wa Mwana wa Mungu, M&M 107:2–4 .
Haki za ukuhani zimeungana na hazitenganishwi na nguvu za mbinguni, M&M 121:36 .
Hakuna nguvu au uwezo unaoweza au upaswao kudumishwa kwa njia ya ukuhani isipokuwa tu kwa ushawishi na upendo usio unafiki, M&M 121:41 .
Kila mwanaume muumini wa kanisa mwenye kustahili anaweza kupokea ukuhani, TR 2 .