Misaada ya Kujifunza
Dera ya kifuani


Dera ya kifuani

Maandiko yanataja aina mbili za dera ya kifuani: (1) Ni vazi ama silaha ya sehemu ya mbele inayomlinda askari. Katika maana ya ishara, Watakatifu wanapaswa kuvaa dirii ya haki ili kujikinga wenyewe dhidi ya maovu (Isa. 59:17; Efe. 6:14). (2) Ni kipande cha vazi kinachovaliwa na kuhani mkuu katika sheria ya Musa (Ku. 28:13–30; 39:8–21). Ilitengenezwa kwa kitani nzuri na kilibeba mawe ya vito kumi na viwili. Wakati mwingine inaelezwa kuwa katika uhusiano na Urimu na Thumimu (M&M 17:1; JS—H 1:35, 42, 52).