Msaada wa Masomo
Mbinguni
iliyopita inayofuata

Mbinguni

Neno mbinguni lina maana mbili za msingi katika maandiko. (1) Ni mahali ambapo Mungu huishi na nyumbani kwa baadaye Watakatifu (Mwa. 28:12; Zab. 11:4; Mt. 6:9). (2) Ni anga liizungukalo dunia (Mwa. 1:1, 17; Ku. 24:10). Mbinguni ni wazi kabisa kuwa siyo peponi, ambapo ni mahali pa muda kwa ajili ya roho aminifu za wale wote walioishi na kufa katika dunia hii. Yesu Kristo alitembelea peponi baada ya kifo Chake msalabani, lakini katika siku ya tatu alimjulisha Maria kwamba Yeye bado alikuwa Hajaenda kwa Baba (Lk. 23:39–44; Yn. 20:17; M&M 138:11–37).