Misaada ya Kujifunza
Meshaki


Meshaki

Katika Agano la Kale, Shadraki, Meshaki, na Abednego walikuwa vijana watatu wa Kiisraeli, ambao, pamoja na Danieli, waliletwa katika kasri ya Nebukadneza, mfalme wa Babilonia. Jina la Meshaki Kiebrania lilikuwa Mishaeli. Vijana hawa wanne walikataa kujichafua wao wenyewe kwa kula chakula na mvinyo wa mfalme (Dan. 1). Shadraki, Meshaki, na Abednego walitupwa katika tanuri ya moto mkali na mfalme, lakini kimiujiza wakaokolewa (Dan. 3).