Misaada ya Kujifunza
Sinai, Mlima


Sinai, Mlima

Mlima katika Rasi ya Sinai karibu na mahali ambapo Musa na Waisraeli walipiga kambi miezi mitatu baada ya kuondoka kwao Misri; pia huitwa Mlima Horebu (Ku. 3:1). Hapa ndipo Mungu alipompa Musa sheria Yake kwa ajili ya nyumba ya Israeli; hapa pia walijenga hema (Ku. 19:2; 20:18; 24:12; 32:15).