Misaada ya Kujifunza
Reubeni


Reubeni

Katika Agano la Kale, ni mwana mkubwa wa Yakobo na Lea (Mwa. 29:32; 37:21–22, 29; 42:22, 37). Ingawa Reubeni alikuwa mzaliwa wa kwanza, alipoteza haki yake ya Uzaliwa wa Kwanza kwa sababu ya dhambi (Mwa. 35:22; 49:3–4).

Kabila la Reubeni

Baraka za Yakobo kwa Reubeni zinapatikana katika Mwanzo 49:3 na Kumbukumbu la Torati 33:6. Idadi ya kabila taratibu ilipungua, na ingawa kabila liliendelea kuwepo, lilipungua umuhimu wake kisiasa. Haki ya uzaliwa wa kwanza ya Reubeni ikamwendea Yusufu na wanawe kwa sababu Yusufu alikuwa mwana wa kwanza wa mke wa pili wa Yusufu, Raheli (1 Nya. 5:1–2).