Misaada ya Kujifunza
Yusufu wa Arimathaya


Yusufu wa Arimathaya

Yusufu wa Arimathaya alikuwa mshirika wa Sanhedrini, mwanafunzi wa Kristo, na Muisraeli aliyekuwa tajiri na mwaminifu ambaye hakushiriki katika kumhukumu Bwana wetu. Baada ya Kusulubiwa, Yusufu aliomba mwili wa Mwokozi aliufunga katika nguo zilizo safi na akamweka katika kaburi lake mwenyewe la mfano wa pango (Mt. 27:57–60; Mk. 15:43–46; Lk. 23:50–53; Yn. 19:38–42).