Msaada wa Masomo
Toba, Tubu


Toba, Tubu

Badiliko la mawazo na moyo ambalo huleta mtazamo mpya kwa Mungu, kwa mtu mwenyewe, na maisha kwa ujumla. Toba humaanisha kwamba mtu hugeuka kabisa kutoka katika uovu na kugeuza moyo wake na mapenzi yake kwa Mungu, akijikabidhi katika amri na mapenzi ya Mungu na kutupa dhambi. Toba ya kweli huja kutokana na upendo kwa Mungu na tamaa ya dhati ya kutii amri zake. Watu wote wenye kuwajibika wamefanya dhambi na lazima watubu ili wapate kukua kuelekea katika wokovu. Ni kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo pekee toba yetu inaweza kuwa na nguvu na kukubaliwa na Mungu.