Misaada ya Kujifunza
Shule ya Manabii


Shule ya Manabii

Katika Kirtland, Ohio, (Marekani), katika wakati wa majira ya baridi ya mwaka 1832–1833, Bwana alimwamuru Joseph Smith kuanzisha shule kwa madhumuni ya kuwafundisha ndugu viongozi wa kanisa mambo yote yahusuyo injili na ufalme wa Mungu. Viongozi wengi wa mwanzoni wa Kanisa walikuja kutoka miongoni mwa wale waliohudhuria shule hii. Shule nyingine ya manabii au wazee iliendeshwa na Parley P. Pratt katika Wilaya ya Jackson, Missouri (M&M 97:1–6). Shule za aina hiyo hiyo zilianzishwa muda mfupi tu baada ya Watakatifu kuhamia magharibi; hata hivyo, hizi zilikatizwa muda mfupi tu. Kufundisha injili siku hizi kunafanyika majumbani, katika akidi za ukuhani na makundi mengine kadha wa kadha na kupitia shule za Kanisa na seminari na madarasa rasmi ya mafundisho.