Misaada ya Kujifunza
Kuhani Mkuu


Kuhani Mkuu

Ofisi katika ukuhani. Maandiko huzungumza juu ya “kuhani mkuu” katika maana mbili: (1) ofisi katika Ukuhani wa Melkizedeki; na (2) chini ya sheria ya Musa, ni ofisa msimamizi wa Ukuhani wa Haruni.

Maana ya kwanza hutumika kwa Yesu Kristo kama Kuhani Mkuu maarufu. Adamu na mapatriaki wote pia walikuwa makuhani wakuu. Siku hizi, makuhani wakuu watatu wasimamizi huunda Urais wa Kanisa na huwasimamia makuhani wengine wote na waumini wa Kanisa. Nyongeza ya wanaume wengine wenye kustahili hutawazwa kuwa makuhani wakuu kulingana na utaratibu kote katika Kanisa leo. Makuhani wakuu waweza kuitwa, kusimikwa, na kutawazwa kuwa maaskofu (M&M 68:19; 107:69–71).

Katika maana ya pili, chini ya torati ya Musa, ofisa msimamizi wa Ukuhani wa Haruni aliitwa kuhani mkuu. Ofisi hii ilirithiwa na ilikuja kupitia kwa mzaliwa wa kwanza miongoni mwa familia ya Haruni, Haruni mwenyewe akiwa kuhani mkuu wa kwanza wa ukuhani wa Haruni (Ku. 28–29; Law. 8; M&M 84:18).