Misaada ya Kujifunza
Kornelio


Kornelio

Akida katika Kaisaria, aliyebatizwa na Petro (Mdo. 10). Yawezekana kuwa yeye alikuwa Myunani wa kwanza kujiunga na Kanisa pasipo kwanza kuongelewa katika dini ya Kiyahudi. Ubatizo wa Kornelio na familia yake uliashiria kufunguka kwa njia kwa injili kuhubiriwa kwa Wayunani. Petro, Mtume kiongozi, aliyeshikilia funguo za ufalme wa Mungu duniani kwa wakati huo, alielekeza mahubiri haya.