Misaada ya Kujifunza
Ibada


Ibada

Kanuni au taratibu takatifu za kidini. Ibada inakuwa na matendo ambayo yana maana za kiroho. Ibada pia yaweza kumaanisha sheria na taratibu za Mungu.

Ibada katika Kanisa hujumuisha huduma kwa wagonjwa (Yak. [Bib.] 5:14–15), kubariki sakramenti (M&M 20:77, 79), ubatizo kwa kuzamishwa (Mt. 3:16; M&M 20:72–74), kubariki watoto (M&M 20:70), kutunukiwa Roho Mtakatifu (M&M 20:68; 33:15), kutunukiwa ukuhani (M&M 84:6–16; 107:41–52), ibada za hekaluni (M&M 124:39), na ndoa katika agano jipya na lisilo na mwisho (M&M 132:19–20).

Ibada zifanywazo kwa niaba ya wafu

Ibada za kidini zifanywazo na mtu aliye hai kwa niaba ya mtu aliyekufa. Ibada hizo huwa na matokeo tu pale wale ambao hufanyiwa ibada hizi wanapozikubali, kushika maagano yanayohusiana, na wanapokuwa wamefungwa kwa yule Roho Mtakatifu wa ahadi. Nazo hufanyika leo ndani ya mahekalu.