Misaada ya Kujifunza
Ibrahimu


Ibrahimu

Mwana wa Tera, aliyezaliwa katika Uru ya Ukaldayo (Mwa. 11:26, 31; 17:5). Nabii wa Bwana ambaye Bwana alifanya naye maagano ya milele, ambayo kupitia kwake mataifa yote ya dunia yamebarikiwa. Ibrahimu mwanzoni aliitwa Abramu.

Kitabu cha Ibrahimu

Maandishi ya Kale yalioandikwa na Ibrahimu ambayo yalikuja kuwa katika milki ya kanisa katika mwaka 1835. Maandishi hayo na maiti kadhaa zilizotiwa mumiani katika makaburi ya watu huko Misri na Antonio Lebolo ambaye aliandika wosia kuwa yawe mali ya Michael Chandler. Chandler aliyaonyesha katika maonyesho ya mwaka 1835 huko Marekani. Baadhi ya marafiki wa Joseph Smith waliyanunua kutoka kwa Chandler na kumpa Nabii, ambaye aliyatafsiri. Baadhi ya maandishi haya sasa yanapatikana katika Lulu ya Thamani Kuu.

Mlango wa 1 umeandikwa juu ya matukio ya Ibrahimu katika Uru ya Ukaldayo, mahali ambako makuhani waovu walijaribu kumtoa yeye kuwa kafara. Mlango wa 2 unaelezea juu ya safari yake ya Kanaani. Bwana alimtokea na kufanya agano naye. Mlango wa 3 umeandikwa kwamba Ibrahimu aliuona uumbaji wote na akatambua mahusianao kati ya sayari za mbinguni. Mlango wa 4–5 ni maandiko mengine juu ya Uumbaji.

Uzao wa Ibrahimu

Watu ambao, kwa utiifu katika sheria na ibada za injili ya Yesu Kristo, hupokea ahadi na maagano yaliyofanywa na Mungu kwa Ibrahimu. Wanaume na wanawake wanaweza kupokea baraka hizi ikiwa wao ni wa uzao halisi wa Ibrahimu au ikiwa wao wamepangwa katika familia yake kwa kuikubali injili na kwa kubatizwa (Gal. 3:26–29; 4:1–7; M&M 84:33–34; 103:17; 132:30–32; Ibr. 2:9–11). Wazao halisi wa Ibrahimu pia wanaweza kupoteza baraka zao kwa kukosa utiifu (Rum. 4:13; 9:6–8).