Misaada ya Kujifunza
Mormoni, Nabii Mnefi


Mormoni, Nabii Mnefi

Nabii Mnefi, jemadari wa jeshi, na mtunza kumbukumbu katika Kitabu cha Mormoni. Mormoni aliishi takribani katika miaka ya 311–385 B.K. (Morm. 1:2, 6; 6:5–6; 8:2–3). Alikuwa kiongozi wa jeshi kwa sehemu kubwa ya maisha yake, kuanzia akiwa na umri wa miaka kumi na mitano (Morm. 2:1–2; 3:8–12; 5:1; 8:2–3). Ammaroni alimwamuru Mormoni kujitayarisha kusimamia historia na kuandika historia (Morm. 1:2–5; 2:17–18). Baada ya kuandika historia ya wakati wa uhai wake yeye mwenyewe, Mormoni aliandika kwa ufupi kutoka mabamba mapana ya Nefi juu ya mabamba ya Mormoni. Baadaye aliyatoa maandiko haya matakatifu kwa mwanawe Moroni. Mabamba haya yalikuwa sehemu ya kumbukumbu ambayo kwayo Joseph Smith alitafsiri Kitabu cha Mormoni.

Maneno ya Mormoni

Kitabu kidogo katika Kitabu cha Mormoni. Katikati ya maneno ya mwisho ya Amaleki katika Kitabu cha Omni na maneno ya mwanzo katika kitabu cha Mosia, Mormoni, mhariri wa kumbukumbu zote, ndiye aliyefanya mwingizo huu mdogo. (Ona “Maelezo Mafupi kuhusu Kitabu cha Mormoni” mwanzoni mwa Kitabu cha Mormoni.)

Kitabu cha Mormoni

Kitabu kilichojitenga ndani ya kitabu cha maandiko kinachojulikana kama Kitabu cha Mormoni. Mlango wa 1–2 huzungumzia juu ya Amaroni, nabii wa Wanefi, akimwamuru Mormoni lini na wapi atakapoyapata mabamba hayo. Pia, vita kuu vinaanza, na Wanefi Watatu walitwaliwa na Bwana kwa sababu ya uovu wa watu. Mlango wa 3–4 huzungumzia juu ya Mormoni akililia toba kwa watu, lakini wao walikwisha kufa ganzi, na uovu mkubwa zaidi ulienea kuliko mwanzoni katika Israeli. Mlango wa 5–6 anaandika pambano la mwisho kati ya Wanefi na Walamani. Mormoni aliuawa pamoja na sehemu kubwa ya taifa la Kinefi. Katika mlango wa 7, kabla ya kifo chake, Mormoni aliwasihi watu—wakati huo, na baadaye—watubu. Katika mlango wa 8–9 anaandika kwamba hatimaye mwana wa Mormoni pekee, Moroni, ndiye aliyebaki hai. Aliandika matukio ya mwisho ya mauti na umwagaji damu, pamoja na mwisho wa watu wa Nefi, na akaandika ujumbe kwa vizazi vya wakati ujao na wasomaji wa historia hii.