Sarafu, noti, hati, au kitu fulani ambacho watu hutumia kama malipo kwa ajili ya bidhaa au huduma. Wakati mwingine ni ishara ya tamaa ya vitu au anasa.
Wale Kumi na Wawili waliambiwa wasichukue chochote kwa ajili ya safari yao, si mkoba, si mkate, wala fedha, Mk. 6:8 .
Petro alimwambia Simoni mchawi ya kwamba pesa zake zingepotelea mbali pamoja naye, Mdo. 8:20 .
Kupenda fedha ndiyo shina la uovu wote, 1Â Tim. 6:10 .
Msitumie fedha kwa yale yasiyo na thamani, 2 Ne. 9:50–51 (Isa. 55:1–2 ; 2 Ne. 26:25–27 ).
Kama watafanya kazi kwa ajili ya fedha, wataangamia, 2Â Ne. 26:31 .
Kabla ya kutafuta utajiri, utafuteni ufalme wa Mungu, Yak. (KM) 2:18–19 .
Makanisa yatasema kwamba kwa fedha zako utasamehewa dhambi zako, Morm. 8:32, 37 .