Kupanga. Mungu, akifanya kazi kupitia Mwanawe, Yesu Kristo, alipanga vitu vya asilia katika asili yake ili kutengeneza mbingu na dunia. Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walimuumba mwanadamu katika mfano Wao (Musa 2:26–27 ).
Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na dunia, Mwa. 1:1 .
Na tufanye mtu kwa mfano wetu, Mwa. 1:26 (Musa 2:26–27 ; Ibr. 4:26 ).
Vitu vyote vilifanywa kwa njia yake, Yn. 1:3, 10 .
Katika yeye vitu vyote viliumbwa vilivyoko mbinguni, Kol. 1:16 (Mos. 3:8 ; Hel. 14:12 ).
Mungu alizifanya ulimwengu kwa Mwana wake, Ebr. 1:2 .
Yesu Kristo aliziumba mbingu na dunia, M&M 14:9 .
Aliwaumba mtu, mme na mke, kwa mfano wake, M&M 20:18 .
Na dunia pasipo idadi nimeziumba, Musa 1:33 .
Kwa njia ya Mwanangu wa pekee niliziumba mbingu, Musa 2:1 .
Mimi, Bwana Mungu niliviumba vitu vyote kiroho kwanza kabla havijawa kikawaida juu ya uso wa dunia, Musa 3:5 .
Mamilioni ya dunia kama hii isingelikuwa mwanzo wa hesabu ya viumbe vyako, Musa 7:30 .
Miungu walipanga na kuzitengeneza mbingu, Ibr. 4:1 .