Mtu aliye mdogo, ambaye bado hajafikia balehe. Akina baba na akina mama wawafundishe watoto wao kutii mapenzi ya Mungu. Watoto hawana dhambi hadi wafikiapo umri wa uwajibikaji (Moro. 8:22 ; M&M 68:27 ).
Watoto ndiyo urithi kutoka kwa Bwana, Zab. 127:3–5 .
Mlee mtoto katika njia impasayo, Mit. 22:6 .
Waacheni watoto wadogo waje kwangu na msiwazuie, Mt. 19:14 .
Watiini wazazi wenu, Efe. 6:1–3 (Kol. 3:20 ).
Pasipo Anguko, Adamu na Hawa wasingelikuwa na watoto, 2 Ne. 2:22–23 .
Wafundisheni watoto kutembea katika ukweli na katika kiasi, Mos. 4:14–15 .
Watoto wadogo wanao uzima wa milele, Mos. 15:25 .
Yesu akawachukua watoto wadogo na kuwabariki, 3Â Ne. 17:21 .
Na watoto wako wote wafundishwe juu ya Bwana, na amani ya watoto wako itakuwa kubwa, 3Â Ne. 22:13 (Isa. 54:13 ).
Watoto wadogo hawahitaji toba au ubatizo, Moro. 8:8–24 .
Watoto wadogo wamekombolewa tangu kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu kwa njia ya Mwanangu wa Pekee, M&M 29:46–47 .
Wazazi yawapasa wawafundishe watoto wao kanuni za injili na desturi zake, M&M 68:25, 27–28 .
Watoto ni watakatifu kwa njia ya upatanisho wa Kristo, M&M 74:7 .
Wazazi wanaamriwa kuwalea watoto wao katika nuru na kweli, M&M 93:40 .
Watoto wanao kufa kabla ya umri wa uwajibikaji wanaokolewa katika ufalme wa selestia, M&M 137:10 .