Misaada ya Kujifunza
Ridhaa ya Wengi


Ridhaa ya Wengi

Kanuni ambayo kwayo waumini wa Kanisa huwakubali wale walioitwa kuhudumu katika Kanisa pamoja na maamuzi mengine ya Kanisa ambayo yanahitaji kuungwa mkono na waumini, kwa kawaida huonyeshwa kwa kuinua mkono wa kuume.

Yesu Kristo husimama kama kiongozi wa Kanisa Lake. Kupitia mwongozo wa Roho Mtakatifu, Yeye huwaelekeza viongozi wa Kanisa katika matendo na maamuzi muhimu. Hata hivyo, waumini wote wa Kanisa wanayo haki na nafasi ya kuyakubali, au kutoyakubali matendo na maamuzi ya viongozi wao.