Misaada ya Kujifunza
Lawi


Lawi

Katika Agano la Kale, ni mwana wa tatu wa Yakobo na Lea (Mwa. 29:34; 35:23). Lawi akawa baba wa mmojawapo wa makabila ya Israeli.

Kabila la Lawi

Yakobo akambariki Lawi na wazao wake (Mwa. 49:5–7, 28). Wazao wa Lawi walihudumu katika mahali patakatifu pa Israeli (Hes. 1:47–54). Haruni alikuwa Mlawi, na wazao wake walikuwa makuhani (Ku. 6:16–20; 28:1–4; 29). Walawi waliwasaidia wale makuhani, wana wa Haruni (Hes. 3:5–10; 1 Fal. 8:4). Wakati mwingine walikuwa kama wanamuziki (1 Nya. 15:16; Neh. 11:22); walichinja dhabihu (2 Nya. 29:34; Ezra 6:20); na kwa ujumla walisaidia katika kazi za hekaluni (Neh. 11:16). Walawi waliwekwa rasmi kwa huduma ya Bwana kutenda ibada kwa ajili ya wana wa Israeli. Walawi wenyewe walitolewa sadaka kwa niaba ya wana wa Israeli (Hes. 8:11–22); hivyo basi wao wakawa mali ya thamani ya Mungu, iliyotolewa Kwake mahali pa mzaliwa wa kwanza (Hes. 8:16). Hawakuwekwa wakfu bali walitakaswa kwa ajili ya ofisi yao (Hes. 8:7–16). Hawakuwa na urithi wa nchi katika Kanaani (Hes. 18:23–24), lakini wao walipokea fungu la kumi (Hes. 18:21), miji arobaini na nane (Hes. 35:6), na haki ya kupokea sadaka za watu katika nyakati za karamu (Kum. 12:18–19; 14:27–29).