Misaada ya Kujifunza
Warumi, Waraka kwa


Warumi, Waraka kwa

Katika Agano Jipya, ni barua ambayo Paulo aliwaandikia Watakatifu katika Roma. Alikuwa akiitafakari safari ya Yerusalemu, ambayo ilikuwa dhahiri ni ya hatari. Kama angeokoa maisha yake, alitumaini baadaye kutembelea Roma. Barua ilikuwa na maana kwa sehemu moja ya kulitayarisha Kanisa huko kumpokea yeye wakati alipoenda. Pia yaweza kuchukuliwa kama yenye taarifa ya mafundisho fulani ambayo yalikuwa yakibishaniwa na kwamba Paulo sasa aliyachukulia kana kwamba mwishowe yamefafanua.

Mlango wa 1 una salamu za Paulo kwa Warumi. Mlango wa 2–11 inajumuisha matamko kadhaa juu ya mafundisho ya imani, matendo, na neema. Mlango 12–16 ina mafundisho ya kimatendo juu ya upendo, kazi, na utakatifu.