Misaada ya Kujifunza
Nuhu, Patriaki wa Biblia


Nuhu, Patriaki wa Biblia

Katika Agano la Kale, ni mwana wa Lameki na ni patriaki wa kumi kutoka kwa Adamu (Mwa. 5:29–32). Alishuhudia juu ya Kristo na alihubiri toba kwa kizazi kilichokuwa kiovu. Watu walipokataa ujumbe wake, Mungu alimwamuru kujenga safina ili kuihifadhi familia yake na wanyama wote wakati dunia ilipofurika ili kuwaangamiza waovu. (Mwa. 6:13–22; Musa 8:16–30). Joseph Smith Nabii alifundisha ya kwamba Nuhu ndiye malaika Gabrieli na ni wa pili kutoka kwa Adamu katika kushikilia funguo za wokovu.