Misaada ya Kujifunza
Asa


Asa

Katika Agano la Kale, ni mfalme wa tatu wa Yuda. Maandiko yameandikwa ya kuwa “moyo wake ulikuwa mkamilifu kwa Bwana siku zake zote” (1 Fal. 15:14). Wakati wa utawala wake aliliunda jeshi imara, na akaweka huru ufalme wake toka kwenye kongwa za Ethiopia, akawaondoa miungu wa uongo, na akawaalika watu kufanya agano la kumtafuta Yehova (1 Fal. 15–16; 2 Nya. 14–16). Hata hiyo, wakati alipokuwa mgonjwa wa miguu yake, hakumwomba Bwana msaada naye akafa (1 Fal. 15:23–24; 2 Nya. 16:12–13).