Misaada ya Kujifunza
Yusufu, Mume wa Maria


Yusufu, Mume wa Maria

Mume wa Maria, mama wa Yesu. Yusufu alikuwa ni wa ukoo wa Daudi (Mt. 1:1–16; Lk. 3:23–38) na aliishi Nazareti. Alimposa Maria. Muda mfupi kabla ya ndoa yao, Maria alitembelewa na malaika Gabrieli, aliyemtangazia kwamba Maria amechaguliwa kuwa mama wa Mwokozi (Lk. 1:26–35). Yusufu pia alipokea ufunuo wa kuzaliwa huku kwa kimungu (Mt. 1:20–25).

Maria alikuwa ndiye mzazi pekee wa kidunia wa Yesu kwa sababu Mungu Baba ndiye aliyekuwa baba wa Yesu. Lakini Wayahudi walimdhania Yusufu kuwa ndiye baba wa Yesu, naye Yesu alimheshimu kama ndiye babaye (Lk. 2:48, 51). Akiwa ameonywa kwa ndoto za mbinguni, Yusufu alilinda uhai wa mtoto mchanga Yesu kwa kukimbilia Misri (Mt. 2:13–14). Baada ya kufa kwa Herode, malaika akamwambia Yusufu amchukue mtoto Kristo warudi Israeli (Mt. 2:19–23).