Neno lililotumika katika maandishi halisi ya Kiyunani linaanisha “chovya” au “zamisha.” Ubatizo kwa uzamisho katika maji na mtu mwenye mamlaka ni ibada ya kwanza ya injili na ni ya muhimu ili kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Hutanguliwa na imani katika Yesu Kristo na katika toba. Ni lazima ufuatiwe na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu ili uweze kuwa kamili (2 Ne. 31:13–14 ). Ubatizo kwa maji na Roho ni muhimu kabla mtu hajaingia katika ufalme wa selestia. Adamu alikuwa mtu wa kwanza kubatizwa (Musa 6:64–65 ). Yesu pia alibatizwa ili kutimiza haki yote na ili kuonyesha njia kwa ajili ya wanadamu wote (Mt. 3:13–17 ; 2 Ne. 31:5–12 ).
Kwa sababu si watu wote duniani hupata nafasi ya kuipokea injili wakiwa duniani, Bwana ametoa mamlaka ubatizo kufanyika kwa watu walio hai kwa niaba ya wale waliokufa. Kwa hiyo, wale waipokeao injili katika ulimwengu wa roho wanaweza kustahili kuingia katika ufalme wa Mungu.
Kubali hivi sasa ili kutimiza haki yote, Mt. 3:15 .
Yesu alikuja na akabatizwa na Yohana, Mk. 1:9 .
Mafarisayo na wanasheria walipinga shauri la Mungu, kwa kutobatizwa, Lk. 7:30 .
Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu, Yn. 3:5 .
Tubuni, na mkabatizwe kila mmoja wenu, Mdo. 2:38 .
Anawaamuru watu wote kwamba lazima wakabatizwe katika jina lake, 2 Ne. 9:23–24 .
Wanadamu lazima wamfuate Kristo, wabatizwe, wampokee Roho Mtakatifu, na kustahmili hadi mwisho ili wapate kuokolewa, 2 Ne. 31 .
Mafundisho ya Kristo ni kwamba wanadamu yawapasa kuamini na kubatizwa, 3 Ne. 11:20–40 .
Yesu alipokwisha kubatizwa, mara akapanda kutoka majini, Mt. 3:16 (Mk. 1:10 ).
Yohana alikuwa akibatiza katika Enoni kwa sababu huko kulikuwa na maji tele, Yn. 3:23 .
Filipo na yule towashi wakateremka ndani ya maji, Mdo. 8:38 .
Tunazikwa pamoja naye kwa ubatizo, Rum. 6:4 (Kol. 2:12 ).
Mfuateni Bwana wenu na Mwokozi wenu chini ndani ya maji, 2 Ne. 31:13 .
Alma, Helamu na wengineo walizikwa ndani ya maji, Mos. 18:12–16 .
Na kisha mtawazamisha ndani ya maji, 3 Ne. 11:25–26 .
Namna sahihi ya ubatizo imeelezwa, M&M 20:72–74 .
Walibatizwa kwa namna ya kuzikwa kwake, wakizikwa ndani ya maji katika jina lake, M&M 76:50–51 .
Adamu alilazwa ndani ya maji na kutolewa kutoka majini, Musa 6:64 .
Ubatizo ni kwa kuzamishwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi, M ya I 1:4 .
Ubatizo kwa ajili ya maondoleo ya dhambi
Baada ya ubatizo huja ondoleo la dhambi zenu kwa moto na kwa Roho Mtakatifu, 2 Ne. 31:17 .
Njooni na mkabatizwe ubatizo wa toba ili mpate kuoshwa kutokana na dhambi zenu, Alma 7:14 .
Wamebarikiwa wao watakao amini na kubatizwa, kwa maana watapokea ondoleo la dhambi zao, 3 Ne. 12:1–2 .
Enendeni na mkayafundishe mataifa yote, mkiwabatiza katika jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Mt. 28:19 (M&M 68:8 ).
Limhi na wengi wa watu wake walikuwa wakitamani kubatizwa, lakini hapakuwa na yeyote katika nchi ile aliyekuwa na mamlaka kutoka kwa Mungu, Mos. 21:33 .
Ninakupa uwezo kwamba utawabatiza, 3 Ne. 11:19–21 .
Ukuhani wa Haruni una funguo za ubatizo kwa kuzamisha kwa ajili ya ondoleo la dhambi, M&M 13 .
Hao ndiyo waliotawazwa nami ili kubatiza katika jina langu, M&M 18:29 .
Sifa zinazotakiwa kwa ajili ya ubatizo
Tubuni, na mkabatizwe katika jina la Mwanangu Mpendwa, 2 Ne. 31:11 .
Lazima mtubu na kuzaliwa tena, Alma 7:14 .
Angalieni kwamba hambatizwi bila kustahili, Morm. 9:29 .
Fundisha wazazi kwamba lazima watubu na wabatizwe na wajinyenyekeze wenyewe, Moro. 8:10 .
Sifa za wale wanaotamani ubatizo zawekwa, M&M 20:37 .
Watoto watabatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zao wafikapo umri wa miaka minane, M&M 68:25, 27 .
Agano lifanywalo kwa njia ya ubatizo
Wale wanaotubu, hujichukulia juu yao jina la Kristo, na wakadhamiria kumtumikia yeye watapokelewa kwa njia ya ubatizo, M&M 20:37 .
Ubatizo kwa ajili ya wafu
Ubatizo siyo kwa ajili ya watoto wachanga
Watoto watabatizwa wakiwa na umri wa miaka minane, M&M 68:27 .
Watoto wote wanaokufa kabla ya miaka ya uwajibikaji wanaokolewa katika ufalme wa selestia, M&M 137:10 .