Misaada ya Kujifunza
Yuda


Yuda

Katika Agano la Kale, ni mwana wa nne wa Yakobo na Lea (Mwa. 29:35; 37:26–27; 43:3, 8; 44:16; 49:8). Yakobo alimbariki Yuda kuwa angekuwa kiongozi wa asili miongoni mwa wana wa Yakobo na kwamba Shilo (Yesu Kristo) angekuwa wa uzao wake (Mwa. 49:10).

Kabila la Yuda

Kabila la Yuda lilichukua uongozi baada ya kuingia na kukaa katika Kaanani. Mpinzani wake mkubwa alikuwa kabila la Efraimu. Musa alilibariki kabila la Yuda (Kum. 33:7). Baada ya utawala wa Sulemani, kabila la Yuda likawa ufalme wa Yuda.

Ufalme wa Yuda

Katika utawala wa Rehoboamu utawala wa Sulemani ulivunjika katika falme mbili tofauti, hasa kwa sababu ya wivu kati ya makabila ya Efraimu na Yuda. Ufalme wa kusini, au ufalme wa Yuda, ilijumuisha ufalme wa Yuda na sehemu kubwa zaidi ya kabila la Benjamini. Yerusalemu yakiwa makao yake makuu. Kwa namna zote ulibaki katika uaminifu zaidi katika kumwabudu Yehova kuliko ulivyofanya ule ufalme wa kaskazini. Yuda ilikuwa imara upande wa kaskazini na mashariki, na mamlaka kuu yalibaki mikononi mwa familia ya Daudi hadi utumwa wa Babilonia. Ufalme wa Yuda ulimudu kudumu kwa miaka 135 baada ya anguko la ufalme wenye watu wengi na wenye nguvu zaidi wa Israeli.

Kijiti cha Yuda

Hii inamaanisha Biblia kama kumbu kumbu ya nyumba ya Yuda (Eze. 37:15–19). Katika siku za mwisho, wakati matawi kadha wa kadha ya nyumba ya Israeli yatakapokuwa yamekusanywa, kumbukumbu zao takatifu pia zitakusanywa pamoja. Kumbu kumbu hizi za maandiko zinakamilishana na kufanya ushuhuda wa umoja kwamba Yesu ndiye Kristo, Mungu wa Israeli na Mungu wa dunia nzima (TJS, Mwa. 50:24–36 [Kiambatisho]; 2 Ne. 3; 29).