Misaada ya Kujifunza
Ezra


Ezra

Kuhani na mwandishi katika Agano la Kale ambaye aliwarejesha Yerusalemu baadhi ya Wayahudi kutoka utumwa wa Babilonia (Ezra 7–10; Neh. 8; 12). Katika mwaka 458 K.K. alipata ruhusa kutoka kwa Artashasta, mfalme wa Uajemi kuwapeleka Yerusalemu mkimbizi yeyote wa Kiyahudi aliyetaka kwenda (Ezra 7:12–26).

Kabla ya wakati wa Ezra, makuhani walikuwa na udhibiti kamili juu ya kusoma mkusanyiko wa maandiko yaliyoandikwa yaliyoitwa “sheria.” Ezra alisaidia kufanya maandiko yapatikane kwa kila Myahudi. Usomaji wa umma wa “kitabu cha sheria” hatimaye ukawa ni sehemu muhimu ya maisha ya taifa la Kiyahudi. Pengine mafundisho makubwa zaidi ya Ezra yalikuja kutokana na mfano wake yeye mwenyewe wa kuutayarisha moyo wake kwa kutafuta sheria za Bwana, kuzitii, na kuifundisha kwa wengine (Ezra 7:10).

Kitabu cha Ezra

Mlango wa 1–6 inaelezea matukio ambayo yalitokea kutoka miaka sitini hadi themanini kabla Ezra hajafika katika Yerusalemu—agizo la Koreshi katika mwaka 537 K.K. na kurejea kwa Wayahudi chini ya Zerubabeli. Mlango wa 7–10 inaonyesha namna Ezra alivyokwenda Yerusalemu. Yeye, pamoja na kikundi chake, walifunga na kusali kwa ajili ya kupata ulinzi. Huko Yerusalemu waliwakuta watu Wayahudi wengi waliokuwa wamekwenda Yerusalemu mapema chini ya Zerubabeli na walikuwa wameoa wanawake nje ya agano na hivyo kujichafua wenyewe. Ezra akawaombea na akawaweka chini ya agano la kuwataliki wake zao wale. Historia ya mwisho ya Ezra inapatikana katika kitabu cha Nehemia.