Misaada ya Kujifunza
Habakuki


Habakuki

Nabii wa Agano la Kale katika Uyahudi aliyenena juu ya hali ya dhambi ya watu inawezekana wakati wa utawala wa Yohoyakini (karibu mwaka 600 K.K.).

Kitabu cha Habakuki

Mlango wa 1 ni majadiliano kati ya Bwana na nabii Wake, sawa sawa na yale yaliyomo katika Yeremia 12 na Mafundisho na Maagano 121. Habakuki alikuwa akisumbuka kwamba waovu wanaonekana kustawi. Katika mlango wa 2 Bwana anamshauri Habakuki kuwa mvumilivu—watu wenye haki lazima wajifunze kuishi kwa imani. Mlango wa 3 unaandikwa sala ya Habakuki ambamo ndani yake anakiri kuwa Mungu ni mwenye haki.