Ruhusa iliyotolewa kwa wanaume duniani walioitwa au kutawazwa ili kutenda kwa ajili ya, na kwa niaba ya Mungu Baba au Yesu Kristo katika kutenda kazi ya Mungu.
Akawapa wanafunzi kumi na wawili uwezo, Mt. 10:1 .
Si ninyi mlionichagua mimi, bali mimi nimewachagua ninyi, na kuwatawaza, Yn. 15:16 .
Nefi na Lehi walihubiri kwa mamlaka makubwa, Hel. 5:18 .
Nefi, mwana wa Helamani, alikuwa mtu wa Mungu, mwenye uwezo mkubwa na mamlaka kutoka kwa Mungu, Hel. 11:18 (3Â Ne. 7:17 ).
Yesu alitoa uwezo na mamlaka kwa Wanefi kumi na wawili, 3 Ne. 12:1–2 .
Joseph Smith aliitwa na kutawazwa na Mungu, M&M 20:2 .
Hakuna atakaye hubiri injili yangu au kulijenga Kanisa langu isipokuwa ametawazwa nayo ijulikane kwa kanisa ya kuwa anayo mamlaka, M&M 42:11 .
Wazee wahubiri injili, wakitenda katika mamlaka, M&M 68:8 .
Ukuhani wa Melkizedeki unayo mamlaka ya kuhudumu katika mambo ya kiroho, M&M 107:8, 18–19 .
Lile lifanywalo kwa mamlaka ya kiungu huwa sheria, M&M 128:9 .