Misaada ya Kujifunza
Yezebeli


Yezebeli

Mwanamke mwovu katika Agano la Kale kutoka nchi ya Foinike. Alikuwa mke wa Ahabu (1 Fal. 16:30–31), mfalme wa Israeli aliyetawala wakati Eliya alipokuwa nabii.

Kuolewa kwa Yezebeli kwa Ahabu, ni tukio moja kubwa zaidi kuliko tukio jingine lolote, lililosababisha kuanguka kwa ufalme wa kaskazini wa Israeli; Yezebeli alianzisha katika Israeli aina mbaya zaidi ya zote ya ibada ya sanamu kutoka katika nchi yake badala ya kumwabudu Yehova (1 Fal. 18:13, 19).

Chapisha