Misaada ya Kujifunza
Injili, Vitabu vya Biblia


Injili, Vitabu vya Biblia

Taarifa nne zilizoandikwa au shuhuda za maisha ya duniani ya Yesu na matukio yahusuyo huduma Yake, iliyomo katika vitabu vinne vya kwanza vya Agano Jipya. Vimeandikwa na Mathayo, Marko, Luka, na Yohana, hizi ni shuhuda zilizoandikwa za maisha ya Kristo. Kitabu cha 3 Nefi katika Kitabu cha Mormoni kinalingana kwa namna nyingi na Injili hizi nne za Agano Jipya.

Vitabu vya Agano Jipya mwanzoni viliandikwa katika Kiyunani. Neno la Kiyunani injili maana yake “habari njema.” Habari njema ni kwamba Yesu Kristo anafanya upatanisho ambao utawakomboa wanadamu wote kutokana na mauti na kumzawadia kila mtu kulingana na matendo yake (Yn. 3:16; Rum. 5:10–11; 2 Ne. 9:26; Alma 34:9; M&M 76:69).

Ona pia Upatanifu wa Injili katika kiambatisho.