Misaada ya Kujifunza
Yuda, Kaka wa Yesu


Yuda, Kaka wa Yesu

Katika Agano Jipya, ni mmoja wa kaka zake Yesu na huenda ndiye mwandishi wa waraka wa Yuda (Mt. 13:55; Yuda 1:1).

Waraka wa Yuda

Kitabu hiki ni nyaraka kutoka kwa Yuda kwenda kwa Watakatifu fulani ambao walikuwa wakidhoofishwa katika imani. Walikuwa wakidhoofishwa na wale miongoni mwao waliokuwa wakidai kuwa ni Wakristo lakini wakitenda ibada za kipagani na wakidai wana ruhusa ya kutotii sheria za maadili. Yuda alitamani kuwaamsha Watakatifu juu ya hali yao ya hatari ya kiroho na kuwatia moyo ili wabaki kuwa waaminifu.

Mistari kadhaa muhimu katika Kitabu cha Yuda ni mstari wa 6, ambayo unakumbusha vita vya mbinguni na kutupwa nje kwa Lusiferi na malaika zake kutoka katika hali ile kabla ya kuzaliwa (Ibr. 3:26–28), na mstari 14–15, ambayo inauelezea unabii uliofanywa na Henoko.