Misaada ya Kujifunza
Hema


Hema

Nyumba ya Bwana, kituo cha kuabudu cha Waisraeli wakati wa kuhama Kutoka Misri. Hema hili kwa kweli lilikuwa ni hekalu linalohamishika na walikuwa wanaweza kulibomoa na kulijenga tena upya. Wana wa Israeli walilitumia hema hadi walipojenga hekalu la Sulemani (M&M 124:38).

Mungu alimfunulia Musa ramani ya hema (Ku. 26–27), na wana wa Israeli walilijenga kulingana na ramani hiyo (Ku. 35–40). Wakati hema lilipokwisha kujengwa, wingu liliifunika hema hilo, na utukufu wa Bwana ukaijaza hema (Ku. 40:33–34). Wingu lilikuwa ni ishara ya uwepo wa Mungu. Usiku, lilikuwa na sura ya moto. Wakati wingu lilipokaa juu ya hema, wana wa Israeli walifanya kambi. Lilipoondoka nao waliondoka pamoja nalo (Ku. 40:36–38; Hes. 9:17–18). Wana wa Israeli waliibeba ile hema wakati wa kutangatanga kwao jangwani na katika utekaji wa nchi ya Kanani. Baada ya utekaji, hema iliwekwa katika Shilo, sehemu ambayo Bwana aliichagua (Yos. 18:1). Baada ya wana wa Israeli kujenga hekalu la Sulemani, hema ilipotea kabisa katika historia.

Bwana na Isaya walitumia hema kama ishara ya miji ya Sayuni na Yerusalemu katika wakati wa Ujio wa Pili wa Bwana (Isa. 33:20; Musa 7:62).