Misaada ya Kujifunza
Mana


Mana

Vipande vidogo, vya mviringo vya aina ya chakula chenye ladha ya asali (Ku. 16:14–31) au mafuta mapya (Hes. 11:7–8). Bwana alikitoa kwa ajili ya kuwalisha mwana wa Israeli wakati wa miaka yao arobaini nyikani (Ku. 16:4–5, 14–30, 35; Yos. 5:12; 1 Ne. 17:28).

Wana wa Israeli walikiita mana (au man-hu katika Kiebrania)—ambayo maana yake ni “Nini hiki?”—kwa sababu hawakujua ni kitu gani (Ku. 16:15). Pia kiliitwa “chakula cha malaika” na “mkate kutoka mbinguni” (Zab. 78:24–25; Yn. 6:31). Kilikuwa ni mfano wa Kristo, ambaye angekuwa Mkate wa Uzima (Yn. 6:31–35).