Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho Ona pia Kanisa, Ishara za Kanisa la Kweli; Kanisa, Jina la; Kanisa la Yesu Kristo; Urejesho wa Injili Jina lililotolewa kwa Kanisa la Kristo katika siku za mwisho ili kutofautisha na Kanisa katika vipindi vingine (M&M 115:3–4). Bwana atamwaga maarifa juu ya Watakatifu wa Siku za Mwisho, M&M 121:33. Joseph Smith ni nabii na mwonaji wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, M&M 127:12. Siku ile kuu ya Bwana i karibu kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho, M&M 128:21, 24. Joseph Smith amesaidia kuwakusanya Watakatifu wa Siku za Mwisho, M&M 135:3. Makundi ya Watakatifu wa Siku za Mwisho yaundwe kwa ajili ya safari ya kwenda nchi ya magharibi ya Marekani, M&M 136:2. Sheria za ndoa zinafafanuliwa kwa ajili ya Watakatifu wa Siku za Mwisho, TR 1. Ukuhani unatolewa kwa wanaume wote wenye kustahili walio waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, M&M TR—2. Maelezo ya juu ya Ono la Kwanza kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho yatolewa, JS—H 1:1.