Misaada ya Kujifunza
Mtume


Mtume

Katika Kiyunani, Mtume maana yake “mtu aliyetumwa.” Kilikuwa ni cheo ambacho Yesu aliwapa wale Kumi na Wawili ambao Yeye aliwachagua na kuwatawaza kuwa wanafunzi Wake wa karibu sana na wasaidizi wake wakati wa huduma Yake hapa duniani (Lk. 6:13; Yn. 15:16). Aliwatuma kumwakilisha Yeye na kuhudumu kwa niaba Yake baada ya kupaa Kwake mbinguni. Zamani na katika Akidi ya Mitume Kumi na Wawili katika Kanisa lililorejeshwa leo, Mtume ni shahidi maalumu wa Yesu Kristo ulimwenguni kote ili kushuhudia juu ya uungu Wake na ufufuko Wake kutoka kwa wafu (Mdo. 1:22; M&M 107:23).

Uteuzi wa Mitume

Mitume huchaguliwa na Bwana (Yn. 6:70; 15:16).