Msaada wa Masomo
Ishara
iliyopita inayofuata

Ishara

Tukio au jambo ambalo watu wanalielewa kuwa ni ushahidi au thibitisho wa kitu fulani. Ishara kwa kawaida ni ono la kimuujiza kutoka kwa Mungu. Shetani pia anao uwezo wa kuonyesha ishara katika hali fulani. Watakatifu yawapasa kutafuta vipawa vya Roho lakini hawapaswi kutafuta ishara ili kuridhisha udadisi au kudumisha imani yao. Ila Bwana atatoa ishara kama Yeye aonavyo kuwa sahihi kwa wale wanaoamini (M&M 58:64).