Misaada ya Kujifunza
Lusiferi


Lusiferi

Jina hili maana yake “Mwenye Kungʼara” au “Mbebanuru.” Pia hujulikana kama Mwana wa Asubuhi. Lusiferi alikuwa mwana wa kiroho wa Baba wa Mbinguni na aliongoza uasi katika maisha kabla ya kuzaliwa duniani. Jina Lusiferi linatokea mara moja tu katika Biblia (Isa. 14:12). Ufunuo wa siku za mwisho hutoa maelezo zaidi juu ya anguko la Lusiferi (M&M 76:25–29).