Msaada wa Masomo
Torati ya Musa
iliyopita inayofuata

Torati ya Musa

Mungu alitoa sheria kwa nyumba ya Israeli kupitia kwa Musa ili kuwa badala ya ile sheria ya juu zaidi ambayo walishindwa kuitii (Ku. 34; TJS, Ku. 34:1–2; TJS, Kum. 10:2 [Kiambatisho]). Torati ya Musa ilikuwa na kanuni nyingi, masharti, ibada, matambiko, na ishara nyingi za kuwakumbusha watu kazi na wajibu wao. Ilijumuisha sheria ya tabia njema, maadili, dini, na amri za kimwili na za matendo—ikiwa ni pamoja na dhabihu (Law. 1–7)—ambazo zilikusudiwa kuwakumbusha juu ya Mungu na wajibu wao kwake Yeye (Mos. 13:30). Imani, toba, ubatizo katika maji, na ondoleo la dhambi zilikuwa ni sehemu ya torati, kama zilivyokuwa Amri Kumi na amri nyingine nyingi za maadili ya hali ya juu na tabia njema. Sehemu kubwa ya sheria zihusuzo sherehe zilimalizika katika mauti na Ufufuko wa Yesu Kristo, ambao ulihitimisha dhabihu kwa kumwaga damu (Alma 34:13–14). Torati ilisimamiwa chini ya Ukuhani wa Haruni na ilikuwa ni injili ya matayarisho ili kuwaleta kwa Kristo wenye kuifuata.