Misaada ya Kujifunza
Wayahudi


Wayahudi

Wayahudi wanaweza kuwa (1) wazao wa Yuda, mmoja wa wana kumi na wawili wa Yakobo, (2) watu wa kale wa ufalme wa kusini wa Yuda, au (3) watu wenye kushika dini, staili za maisha, na mila za dini ya Kiyahudi lakini aweza kuwa au asiwe Myahudi kwa kuzaliwa. Imekuwa ni kitu cha kawaida kutumia neno Myahudi kwa kuwaonyesha wazao wote wa Yakobo, lakini hili ni kosa. Ni lazima litumike kwa wale walio wa ufalme wa Yuda au, hususani zaidi kwa siku hizi, wale walio wa kabila la Yuda na washirika wake.