Misaada ya Kujifunza
Misri


Misri

Nchi katika kona ya kaskazini mashariki ya Afrika. Sehemu kubwa ya Misri ni jangwa na isiyokaliwa na watu. Wakazi wake wengi huishi katika Bonde la Nile, ambalo lina urefu wa kiasi cha maili 550 (kilometa 890).

Misri ya kale ilikuwa tajiri na yenye kustawi. Miradi mikubwa ya kiuhandisi ilijengwa, ikiwa pamoja na mifereji ya umwagiliaji, miji yenye ngome imara kwa ajili ya ulinzi; na masanamu ya kifalme ya ukumbusho, hususani makaburi ya piramidi na mahekalu, ambayo bado yapo miongoni mwa maajabu ya ulimwengu. Kwa wakati fulani, serikali ya Kimisri ilikuwa katika mfano wa utaratibu wa kipatriaki katika ukuhani (Ibr. 1:21–27).