Misaada ya Kujifunza
Ayubu


Ayubu

Katika Agano la Kale, ni mtu mwadilifu aliyeteseka kwa mateso makubwa lakini alibakia mwaminifu katika imani yake kwa Mungu. Historia yake inasimuliwa katika kitabu cha Ayubu.

Kitabu cha Ayubu

Ingawa kitabu hiki ni juu ya mateso ya Ayubu, hakijibu moja kwa moja swali la kwa nini Ayubu (au mtu mwingine yeyote) anaweza kuteseka kwa maumivu na kupoteza familia yake na mali. Kitabu kinafafanua kwamba kupata mateso maana yake siyo lazima kwamba mtu huyo ametenda dhambi. Bwana anaweza kutumia mateso kwa ajili ya kutupa uzoefu, kutufundisha nidhamu, na kufundisha vile vile kama adhabu (M&M 122).

Kitabu hiki chaweza kugawanywa katika sehemu nne. Mlango wa 1–2 ni utangulizi wa hadithi hii. Mlango wa 3–31 inaelezea mfuatano wa majadiliano kati ya Ayubu na marafiki zake watatu. Mlango wa 32–37 ina mahubiri ya Elihu, rafiki wa nne, ambaye anamshutumu Ayubu kwa sababu nyingine tofauti na zile za marafiki watatu wa kwanza. Mlango wa 38–42 inahitimisha kitabu kwa uhakikisho kwa Ayubu kwamba mwenendo wake wa maisha ulikuwa mwema tangu mwanzo.

Kitabu cha Ayubu hufundisha kwamba kama mtu anao ufahamu sahihi juu ya Mungu na anaishi maisha ambayo yanakubalika kwa Mungu, itakuwa bora kwake kustahimili majaribu yanayokuja juu yake. Imani isiyotindika ya Ayubu inayoonekana wazi katika matamko kama “Japokuwa ataniua, bado nitamtumaini yeye.” (Ayu. 13:15). Ayubu pia ametajwa katika Ezekieli 14:14; Yak. (Bib.) 5:11; Mafundisho na Maagano 121:10.