Misaada ya Kujifunza
Utangulizi


Mwongozo wa Maandiko

Mwongozo wa Maandiko hutoa maana fupi ya mafundisho, kanuni, watu, na mahali vinapopatikana katika Biblia Takatifu, Kitabu cha Mormoni, Mafundisho na Maagano, na Lulu ya Thamani Kuu. Na pia hutoa marejeo muhimu ya kimaandiko kwa ajili ya mafundisho yako kwa kila mada. Mwongozo huu waweza kukusaidia wewe katika mafundisho yako ya maandiko kibinafsi na kifamilia. Unaweza kukusaidia kujibu maswali juu ya injili, kujifunza mada katika maandiko, kutayarisha mahubiri na masomo, na kuongeza maarifa na ushuhuda wa injili.

Mchoro ufuatao unaelezea mfano wa ingizo katika Mwongozo wa Maandiko:

Picha
sample

Dunia

Sayari ambayo juu yake tunaishi, iliumbwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo ili itumiwe na mwanadamu wakati wa kuzaliwa katika mwili wenye kufa na kwa majaribio yake. Hatima yake ni kuwa iliyotukuzwa na kuinuliwa. (M&M 77:1–2; 130:8–9). Dunia itakuwa ni urithi wa milele wa wale walioishi wakistahili fahari ya selestia (M&M 88:14–26). Watafurahia uwepo wa Baba na Mwana (M&M 76:62).

Iliumbwa kwa ajili ya mwanadamu

Kalvari

Kanisa, Lililo Kuu na Lenye Kuchukiza

Mada zipo katika herufi nzito.

Mada zinajumuisha maana kwa ufupi.

Baadhi ya mada zina mada ndogo. Mada hizi ziko katika herufi aina ya mlazo za italiki.

Marejeo ya maandiko ambayo hukusaidia wewe kufahamu maana yapo katika mabano.

Nyakati zingine habari juu ya somo halijumuishwi chini ya mada uliyoiangalia. Neno la herufi mlazo la kiitaliki Tazama hukuelekeza kwenye mada ambako habari zake hupatikana.

Nyakati zingine mada zingine katika mwongozo zinazo habari ambazo zinahusiana na mada ambayo wewe unajifunza. Maneno ya hefuri mlazo ya kiitaliki Ona pia hukuelekeza wewe kwenye mada hizi zinazohusiana nayo.

Marejeo ya kimaandiko yanayofanana yametolewa katika mabano.

Kila rejeo la kimaandiko limetanguliwa na dondoo fupi kutoka andiko au ufupisho wa andiko.

Neno la herufi mlazo la kiitaliki Ona (au Ona pia) likifuatiwa na dashi hii hukuambia wewe kwamba taarifa hiyo inapatikana katika mlango mdogo (“Kanisa la ibilisi”) wa mada kuu (“Ibilisi”).