Misaada ya Kujifunza
Sheria


Sheria

Amri au masharti ya Mungu ambayo juu yake baraka na adhabu zote husimama kote mbinguni na duniani. Wale wanaotii sheria za Mungu hupokea baraka zilizoahidiwa. Joseph Smith Nabii alifundisha ya kuwa watu ni lazima pia watii, waheshimu, na kuzikubali sheria za nchi (M ya I 1:12).

Torati ya Musa ilikuwa ni sheria ya matayarisho ya kuwaleta wanaume na wanawake kwa Kristo. Ilikuwa sheria yenye maamrisho, maelekezo, na ibada. Siku hizi sheria ya Kristo, ambayo inatimiliza torati ya Musa, ni utimilifu wa injili au “sheria kamilifu iliyo ya uhuru” (Yak. [Bib.] 1:25).