Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 42


Sehemu ya 42

Ufunuo uliotolewa katika sehemu mbili kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, 9 na 23 Februari 1831. Sehemu ya kwanza, ina aya ya 1 hadi ya 72, ilipokelewa mbele ya wazee kumi na wawili na ni katika kutimiza ahadi ya Bwana aliyoifanya hapo awali kwamba “sheria” ingelitolewa Ohio (ona sehemu ya 38:32). Sehemu ya pili ina aya ya 73 hadi ya 93. Nabii anaelezea kuwa ufunuo huu ni kama “kukubali sheria ya Kanisa.”

1–10, Wazee wameitwa kuhubiri injili, kubatiza waongofu, na kulijenga Kanisa; 11–12, Ni lazima waitwe na kutawazwa, na watafundisha kanuni za injili zipatikanazo katika maandiko; 13–17, Wao watafundisha na kutoa unabii kwa uwezo wa Roho; 18–29, Watakatifu wanaamriwa wasiue, wasiibe, wasiseme uongo, wasitamani, wasizini, au wasinene maovu dhidi ya wengine; 30–39, Sheria zinazotawala uwekaji wakfu kwa mali yatolewa; 40–42, Majivuno na uvivu vyalaaniwa; 43–52, Wagonjwa wataponywa kwa njia ya huduma na kwa imani; 53–60, Maandiko yanalitawala Kanisa na yatatangazwa kwa ulimwengu; 61–69, Kiwanja cha Yerusalemu Mpya na siri za ufalme zitafunuliwa; 70–73, Mali zilizowekwa wakfu zitumiwe kusaidia maofisa wa Kanisa; 74–93, Sheria zinazotawala uasherati, uzinzi, kuua, kuiba, na kuungama dhambi zinawekwa.

1 Sikilizeni, Enyi wazee wa kanisa langu, ambao mmekusanyika pamoja katika jina langu, hata Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai, Mwokozi wa ulimwengu; kwa sababu mnaliamini jina langu na kushika amri zangu.

2 Tena ninawaambia, sikilizeni na mkasikie na kuitii asheria ambayo nitawapa.

3 Kwani amini ninasema, kama vile wenyewe mlivyokusanyika pamoja kulingana na aamri ambayo niliwaamuru, na bkukubaliana juu ya jambo hili moja, na mmemwomba Baba katika jina langu, hata hivyo nanyi mtapokea.

4 Tazama, amini ninawaambia, ninawapa amri hii ya kwanza, kwamba mtakwenda katika jina langu, kila mmoja wenu, isipokuwa watumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na Sidney Rigdon.

5 Na ninawapatia wao amri kwamba waende kwa muda mfupi, na itatolewa kwa uwezo wa aRoho lini wao warudi.

6 Nanyi mtaenenda katika nguvu ya Roho wangu, mkihubiri injili yangu, awawili wawili, katika jina langu, mkipaza sauti zenu kama kwa sauti ya tarumbeta, mkilitangaza neno langu kama vile malaika wa Mungu.

7 Na mtaenda kubatiza kwa maji, mkisema: Tubuni ninyi, tubuni ninyi, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

8 Na toka mahali hapa mtaenda katika maeneo ya magharibi; na kadiri mtakavyowapata watakaowapokea ninyi mtajenga kanisa langu katika kila eneo—

9 Hadi wakati utakapokuja itakapofunuliwa kwenu kutoka juu, wakati ambao amji wa bYerusalemu Mpya utatayarishwa, ili muweze ckukusanyika mahali pamoja, ili muweze kuwa dwatu wangu na Mimi nitakuwa Mungu wenu.

10 Na tena, ninawaambia, kwamba mtumishi wangu aEdward Partridge atasimama katika ofisi ambayo nimemteua. Na itakuwa, kwamba kama atavunja sheria bmwingine atateuliwa katika mahali pake. Hivyo ndivyo. Amina.

11 Tena ninawaambia, kwamba haitatolewa kwa yeyote kwenda akuhubiri injili yangu, au kulijenga kanisa langu, isipokuwa bametawazwa na mtu fulani aliye na cmamlaka, na ijulikane kwa kanisa kwamba anayo mamlaka na ametawazwa kwa utaratibu na viongozi wa kanisa.

12 Na tena, awazee, makuhani na waalimu wa kanisa hili bwatafundisha kanuni za injili yangu, ambayo imo katika cBiblia na dKitabu cha Mormoni, ambamo umo utimilifu wa einjili.

13 Na watayashika amaagano na kanuni za kanisa na kuzitenda, na haya yatakuwa mafundisho yao, kama watakavyoelekezwa na Roho.

14 Na Roho atatolewa kwenu kwa asala ya imani; na msipompokea bRoho msifundishe.

15 Na hii yote mtaendelea kutenda kama nilivyowaamuru juu ya kufundisha kwenu, hadi utimilifu wa amaandiko yangu matakatifu yamejulikana.

16 Na wakati mtakapopaza sauti zenu mkiongozwa na aMfariji, mtanena na kutoa unabii kama nionavyo kuwa vyema;

17 Kwa maana, tazama, Mfariji ajua mambo yote, na humshuhudia Baba na Mwana.

18 Na sasa, tazama, nasema kwa kanisa. aUsiue; na yule banayeua hatapata msamaha katika ulimwengu huu, wala katika ulimwengu ujao.

19 Na tena, ninasema, usiue, lakini yule anayeua aatakufa.

20 aUsiibe; kwani na yule aibaye asipotubu atatupwa nje.

21 aUsiseme uongo; yule asemaye uongo na asipotubu atatupwa nje.

22 aMpende mke wako kwa moyo wako wote, na butaambatana na yeye tu na siyo mwingine.

23 Na yule amwangaliaye mwanamke kwa akumtamani anaikana imani, na hatakuwa na Roho; na kama hatatubu atatupwa nje.

24 aUsizini; na yule afanyaye uzinzi, na hatubu, atatupwa nje;

25 Bali yule ambaye amezini na akutubu kwa moyo wake wote, na kusahau, na asitende tena, bmtamsamehe;

26 Lakini akirudia atena, hatasamehewa, bali atatupwa nje.

27 aUsimseme jirani yako uovu, wala usimdhuru.

28 Mnajua sheria zangu juu ya mambo haya zimetolewa katika maandiko yangu; yule atendaye dhambi na hatubu aatatupwa nje.

29 Kama awanipenda butanitumikia na ckushika amri zangu zote.

30 Na tazama, nanyi mtawakumbuka amaskini, na bkuweka wakfu baadhi ya mali zenu kwa ajili ya ckuwasaidia wao, kile mlichonacho kwa kuwasaidia wao, kwa agano na mkataba ambao hauwezi kuvunjwa.

31 Na kadiri amtakavyotoa sehemu ya mali yenu kwa bmaskini, mmenitendea Mimi; na mtaiweka mbele ya caskofu wa kanisa langu na washauri wake, wawili kati ya wazee, au makuhani wakuu, kama vile atakavyowateua na dkuwaweka rasmi kwa madhumuni hayo.

32 Na itakuja kutokea, kwamba baada ya kuwa imewekwa mbele ya askofu wa kanisa langu, na baada ya kuwa amepokea shuhuda hizi juu ya akuwekwa wakfu kwa mali ya kanisa langu, kwamba haiwezi kuchukuliwa kutoka kanisani, kulingana na amri zangu, kila mtu atafanywa bawajibike kwangu, cmtumishi juu ya mali yake mwenyewe, au ile ambayo ameipokea kwa kuweka wakfu, ilimradi ni ya kutosha kwake mwenyewe na kwa dfamilia yake.

33 Na tena, kama kutakuwa na mali katika mikono ya kanisa, au mmoja wa watu wake, zaidi kuliko mahitaji yao baada ya uwekaji wakfu huu wa kwanza, ambayo ni amabaki yatawekwa wakfu kwa askofu, nayo yatatunzwa kwa kuwahudumia wale wasionacho, mara kwa mara, kusudi kila mtu mwenye shida aweze kupewa vya kutosha na kupokea kulingana na mahitaji yake.

34 Kwa hivyo, mabaki yatatunzwa ghala ni mwangu, kwa kuwahudumia maskini na wenye shida, kama itakavyoamriwa na baraza kuu la kanisa, na askofu na baraza lake;

35 Na kwa madhumuni ya ununuzi wa ardhi kwa manufaa ya jumuia ya kanisa langu, na ujenzi wa nyumba za kuabudu, na ujenzi wa aYerusalemu Mpya ambayo itafunuliwa hapo baadaye—

36 Ili watu wangu wa agano waweze kukusanywa mahali pamoja katika siku ile wakati anitakapokuja kwenye bhekalu langu. Na hii nitafanya kwa ajili ya wokovu wa watu wangu.

37 Na itakuwa, kwamba yule ambaye hutenda dhambi na hatubu aatatupwa nje ya kanisa, na hatapokea tena kile ambacho alikiweka bwakfu kwa maskini na wenye shida wa kanisa langu, au kwa maneno mengine, kwangu Mimi—

38 Kwani kadiri amlivyomtendea mmojawapo wa hawa, mmenitendea Mimi.

39 Kwani itakuwa, kwamba kile nilichokinena kwa vinywa vya manabii wangu kitatimizwa; kwa kuwa nitaweka wakfu utajiri wa wale ambao huikumbatia injili yangu miongoni mwa Wayunani kwa maskini wa watu wangu ambao ni wa nyumba ya Israeli.

40 Na tena, nawe usiwe na amajivuno katika moyo wako; bmavazi yako yawe ya kawaida, na uzuri wao uwe uzuri wa kazi za mikono yako;

41 Na mambo yote yafanyike katika usafi mbele yangu.

42 Usiwe amvivu; kwani yule aliye mvivu hatakula mkate wala kuvaa mavazi ya mfanya kazi.

43 Na yeyote miongoni mwenu aliye amgonjwa, na hana imani ya kuponywa, lakini anaamini, alishwe mboga na chakula laini, na kwamba siyo kwa mkono wa adui.

44 Na wazee wa kanisa, wawili au zaidi, wataitwa, na watamwombea kwa kuweka amikono yao juu yao katika jina langu; na kama bwatakufa, watakufa kwangu, na kama wataishi, wataishi kwangu.

45 Nawe autaishi pamoja katika bupendo, kwa kiasi kwamba cutalia kwa upotevu wa wale wanaokufa, na hasa kwa wale ambao hawana dtumaini la ufufuko mtukufu.

46 Na itakuwa kwamba wale wanaokufa kwangu hawataonja amauti, kwani itakuwa bvyema kwao;

47 Na wale wasiokufa kwangu, ole wao, kwani kifo chao ni kichungu.

48 Na tena, itakuwa kwamba yule aliye na aimani kwangu ya bkuponywa, na chakuteuliwa kufa, ataponywa.

49 Yule aliye na imani ya kuona ataona.

50 Yule aliye na imani ya kusikia atasikia.

51 Kiwete aliye na imani ya kuruka ataruka.

52 Na wale ambao hawana imani ya kufanya mambo haya, lakini wanayo imani na Mimi, wanao uwezo wa kuwa awana wangu; ilimradi hawavunji sheria zangu wewe butaubeba udhaifu wao.

53 Utasimama katika mahali pa ausimamizi wako.

54 Usichukue vazi la ndugu yako; nawe utalipa kwa kile utakachokipokea kutoka kwa ndugu yako.

55 Na kama autapata zaidi kuliko mahitaji yako, utaitoa katika bghala yangu, kwamba yote yaweze kufanyika kulingana na kile nilichosema.

56 Nanyi mtaniomba, na amaandiko yangu yatatolewa kama nilivyonena, nayo byatatunzwa katika usalama;

57 Na ni vyema kwamba yawapasa kunyamaza juu yake, na msiyafundishe hadi mtakapoyapokea katika ukamilifu.

58 Na ninatoa kwenu ninyi amri kwamba ndipo mtayafundisha kwa watu wote; kwani yatafundishwa kwa mataifa ayote, makabila, lugha na watu.

59 Utayachukua mambo ambayo umeyapokea, ambayo yametolewa kwako katika maandiko yangu kuwa sheria, kuwa sheria ya kulitawala kanisa langu;

60 Na yule ambaye ahuyatenda kulingana na mambo haya ataokolewa, na yule ambaye hayatendi batahukumiwa kama ataendelea hivyo.

61 Ikiwa utaomba, nawe utapokea aufunuo juu ya ufunuo, bmaarifa juu ya maarifa, ili uweze kujua csiri na mambo ya damani—yale ambayo huleta eshangwe, yale ambayo huleta uzima wa milele.

62 Nawe utaomba, na itafunuliwa kwako kwa wakati wangu mahali ambapo aYerusalemu Mpya itajengwa.

63 Na tazama, itakuwa kwamba watumishi wangu watatumwa mashariki na magharibi, kaskazini na kusini.

64 Na hata sasa, na yule aendaye mashariki awafundishe wale watakaoongoka kukimbilia amagharibi, na hii ni katika matokeo ya kile ambacho chaja juu ya ulimwengu, na bmakundi maovu ya siri.

65 Tazama, nawe utatii mambo haya yote, na thawabu yako itakuwa kubwa; kwani kwako imetolewa kujua siri za ufalme, bali kwa walimwengu haikutolewa kujua.

66 Nanyi mtatii sheria ambazo mmezipokea na kuwa waaminifu.

67 Na hapo baadaye mtapokea amaagano ya kanisa, kiasi cha kuwatosha ninyi kuendelea, kote hapa na katika Yerusalemu Mpya.

68 Kwa hivyo, yule ambaye amepungukiwa ahekima, na aniombe mimi, na nitampa yeye kwa ukarimu na sitamkemea.

69 Inueni mioyo yenu na mfurahi, kwani kwenu aufalme, au kwa maneno mengine, bfunguo za kanisa zimetolewa. Hivyo ndivyo. Amina.

70 aMakuhani na bwalimu watapewa cusimamizi, hata kama waumini.

71 Na wazee au makuhani wakuu ambao wameteuliwa kumsaidia askofu kama washauri katika mambo yote, familia zao zita saidiwa kwa mali iliyowekwa awakfu kwa askofu, kwa ajili ya maskini, na kwa madhumuni mengineyo, kama ilivyotajwa hapo awali;

72 Au watapokea ujira kwa huduma zao zote, iwe kwa usimamizi au vinginevyo, kama itakavyoonekana vema au kuamuliwa na washauri na askofu.

73 Na askofu pia, atapokea msaada wake, au malipo ya haki kwa huduma zake zote katika kanisa.

74 Tazama, amini ninawaambia, kwamba mtu yeyote miongoni mwenu, atakayemwacha mwenzi wake kwa sababu ya auasherati, au kwa maneno mengine, kama watathibitisha mbele yenu kwa unyenyekevu wote wa moyo kwamba hiyo ndiyo sababu, msiwatupe nje kutoka miongoni mwenu;

75 Lakini kama mtapata mtu yeyote amemwacha mwenzi wake kwa ajili ya auzinzi, naye ndiye mkosaji, na wenzi hao wanaishi, bwatupwe nje kutoka miongoni mwenu.

76 Na tena, ninawaambia, kwamba mtakuwa awaangalifu, kwa kuwahoji, ili msimpokee yeyote wa aina hiyo miongoni mwenu kama wameoa au kuolewa;

77 Na kama hawajaoa au kuolewa, watubu dhambi zao zote, au msiwapokee.

78 Na tena, mtu yeyote aliye wa kanisa hili la Kristo, atazishika na kutii amri zote na maagano ya kanisa.

79 Na itakuwa, kwamba kama mtu yeyote miongoni mwenu aataua atolewe na kushughulikiwa kulingana na sheria za nchi; kwani kumbukeni kwamba yeye hana msamaha; na itathibitika kulingana na sheria za nchi.

80 Na kama mwanaume yeyote au mwanamke atazini, ashtakiwe mbele ya wazee wawili wa kanisa, au zaidi, na kila neno litathibitika dhidi yake kwa mashahidi wawili wa kanisa, na si kwa adui; lakini kama kuna zaidi ya wawili ni bora zaidi.

81 Lakini yeye atahukumiwa kwa vinywa vya mashahidi wawili; na wazee wataliweka shauri mbele ya kanisa, na kanisa litanyosha mkono dhidi yake, ili kwamba waweze kushughulikiwa kulingana na sheria ya Mungu.

82 Na kama yawezekana, askofu ni muhimu awepo pia.

83 Na hivi ndivyo mtakavyofanya katika kila shauri litakalokuja mbele yenu.

84 Na kama mwanaume au mwanamke atapora, huyo atolewe kwa sheria ya nchi.

85 Na kama mwanaume au mwanamke aataiba, hivyo atolewe kwa sheria ya nchi.

86 Na kama mwanaume au mwanamke aatadanganya, atolewe kwa sheria za nchi.

87 Na mwanaume au mwanamke atafanya aina yoyote ya uovu, huyo atatolewa kwa sheria, hata ile ya Mungu.

88 Na kama akaka au dada yako bamekukosea, utamchukua yeye na kati yenu ninyi peke yenu; na kama catakiri mtapaswa kupatana.

89 Na kama hakiri mtoe kwa kanisa, siyo kwa waumini, bali kwa wazee. Na itafanyika katika mkutano, na kwamba siyo mbele ya ulimwengu.

90 Na kama kaka au dada yako amewakosea wengi, na aakavipiwe mbele ya wengi.

91 Na kama mtu yeyote anakosea wazi, na akemewe wazi, ili aweze kuaibika. Na kama hakiri, atolewe kwa sheria ya Mungu.

92 Kama mtu yeyote anakosea kwa siri, akanywe kwa siri, ili aweze kupata nafasi ya kukiri kwa siri kwake yeye aliyemkosea, na kwa Mungu, ili kanisa lisiweze kumfedhehesha.

93 Na hivyo ndivyo mtakavyojiendesha katika mambo yote.