Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 25


Sehemu ya 25

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Harmony, Pennsylvania, Julai 1830 (ona kichwa cha habari cha sehemu ya 24). Ufunuo huu ulionyesha mapenzi ya Bwana kwa Emma Smith, mke wa Nabii.

1–6, Emma Smith, bibi mteule, anaitwa kumsaidia na kumfariji mume wake; 7–11, Yeye pia ameitwa kuandika, kuelezea maandiko, na kuchagua nyimbo; 12–14, Wimbo wa mwenye haki ni sala kwa Bwana; 15–16, Kanuni za Utii katika ufunuo huu inatumika kwa wote.

1 Sikiliza sauti ya Bwana Mungu wako, wakati ninapoongea na wewe, Emma Smith, binti yangu; kwani amini ninakuambia, wale wote ambao ahuipokea injili yangu ni wana na mabinti katika bufalme wangu.

2 Ufunuo ninautoa kwako kuhusiana na mapenzi yangu; na endapo wewe utakuwa mwaminifu na akuenenda katika njia za bhaki mbele zangu, nitayalinda maisha yako, na wewe utapata curithi katika Sayuni.

3 Tazama, adhambi zako zimesamehewa, na wewe u bibi mteule, ambaye bnimekuita.

4 Usinungʼunike kwa sababu ya vitu ambavyo wewe hujaviona, kwani vimezuiliwa kwako na kwa ulimwengu, ambayo ni hekima kwangu katika wakati ujao.

5 Na ofisi ya wito wako itakuwa kwa afaraja ya mtumishi wangu, Joseph Smith, Mdogo, mume wako, katika mateso yake, kwa maneno ya faraja, katika roho wa unyenyekevu.

6 Na wewe utakwenda naye wakati wa kuondoka kwake, na uwe mwandishi wake, wakati pakiwa hakuna mtu wa kuandika kwa ajili yake, ili niweze kumtuma mtumishi wangu, Oliver Cowdery, kokote nipendako.

7 Na wewe autatawazwa chini ya mikono yake kuyaelezea maandiko, na kushawishi kanisa, kadiri Roho wangu atakavyokujalia.

8 Kwani yeye ataweka amikono yake juu yako, nawe utampokea Roho Mtakatifu, na muda wako utatumika katika kuandika, na kujifunza mengi.

9 Nawe hutakiwi kuogopa, kwani mume wako atakusadia katika kanisa; kwani kwao ndiyo awito wake, ili kwamba mambo yote yaweze bkufunuliwa kwao, lolote nitakalo kulingana na imani yao.

10 Na amini ninakuambia wewe kwamba uyaweke kando amambo ya bulimwengu huu, na ckuyatafuta mambo ya ulimwengu ulio bora.

11 Na itatolewa kwako, pia, kufanya uchaguzi wa anyimbo takatifu, kama itakavyotolewa kwako, zile zenye kunipendeza Mimi, ili ziimbwe katika kanisa langu.

12 Kwani nafsi yangu hufurahia katika anyimbo za bmoyoni; ndiyo, wimbo wa mwenye haki ni sala kwangu Mimi, nayo itajibiwa kwa baraka juu ya vichwa vyao.

13 Kwa hiyo, inua moyo wako na ufurahie, na uyashikilie maagano ambayo umeyafanya.

14 Endelea katika roho wa aunyenyekevu, na jihadhari na bmajivuno. Acha nafsi yako ifurahie katika mume wako, na utukufu ule ambao utakuja juu yake.

15 Shika amri zangu daima, na ataji la bhaki utalipokea. Na bila wewe kufanya hivyo, mahali Mimi nilipo wewe chutaweza kuja.

16 Na amini, amini, ninakuambia, kwamba hii ni asauti yangu kwa wote. Amina.