Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 91


Sehemu ya 91

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, 9 Machi 1833. Nabii kwa wakati huu alikuwa anajishughulisha na tafsiri ya Agano la Kale. Akiwa amefikia kwenye sehemu ya maandishi ya Kale yaitwayo Apokrifa, alimwuliza Bwana na kupokea maelezo haya.

1–3, Apokrifa imetafsiriwa kwa usahihi zaidi ila ina mengi yaliyoongezwa kwa mikono ya wanadamu ambayo siyo ya kweli; 4–6, Inawanufaisha wale wenye kuangazwa na Roho.

1 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana ninyi kuhusu aApokrifa—Kuna mambo mengi yaliyomo ndani yake ambayo ni ya kweli, na imetafsiriwa kwa usahihi sana;

2 Kuna mambo mengi ndani yake ambayo siyo ya kweli, ambayo yameongezwa kwa mikono ya wanadamu.

3 Amini, ninawaambia, kwamba siyo lazima Apokrifa itafsiriwe.

4 Kwa hiyo, yeyote aisomaye, na aafahamu, kwani Roho hufunulia ukweli;

5 Na yeyote atakayeangazwa na aRoho atapata faida kutoka humo;

6 Na yeyote asiyepokea kwa Roho, hawezi kufaidika nayo. Kwa hiyo siyo lazima kwamba kitafsiriwe. Amina.