Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 14


Sehemu ya 14

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa David Whitmer, huko Fayette, New York, Juni 1829. Familia ya Whitmer ilipata kuvutiwa sana katika kutafsiri Kitabu cha Mormoni. Nabii alianzisha makazi yake katika nyumba ya Peter Whitmer Mkubwa, mahali alipokaa hadi kazi ya tafsiri ilipofika kukamilika na haki miliki ya kitabu kilichotarajiwa ilipopatikana. Kati ya wana watatu wa Whitmer, kila mmoja akiwa amepokea ushuhuda wa ukweli wa kazi hiyo, wakawa wamejihusisha sana juu ya mambo ya wajibu wa kila mmoja. Ufunuo huu na mbili zinazofuatia (sehemu ya 15 na 16) zilitolewa kama jibu la maulizo kupitia Urimu na Thumimu. David Whitmer baadaye alikuja kuwa mmoja kati ya Mashahidi Watatu wa Kitabu cha Mormoni.

1–6, Wafanya kazi katika shamba la mizabibu watapata wokovu; 7–8, Uzima wa milele ni zawadi iliyo kubwa ya Mungu; 9–11, Kristo aliumba mbingu na nchi.

1 Kazi akubwa na ya ajabu i karibu kuja miongoni mwa wanadamu.

2 Tazama, Mimi ndimi Mungu; litiini neno langu, lililo hai na lenye nguvu, kali kuliko upanga wenye makali pande mbili, kwa kugawanya viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; kwa hivyo litii neno langu.

3 Tazama, shamba ni jeupe tayari kwa mavuno; kwa hiyo, yeyote atakaye kuvuna na aingize ndani mundu yake kwa nguvu zake, na kuvuna wakati siku ingali, ili aweze kujiwekea hazina ya wokovu usio na mwisho kwa ajili ya nafsi yake katika ufalme wa Mungu.

4 Ndiyo, yeyote atakayeingiza mundu yake na kuvuna, yeye huyo ameitwa na Mungu.

5 Kwa hivyo, kama utaniomba Mimi utapata; kama utabisha utafunguliwa.

6 Tafuta kuanzisha na kustawisha Sayuni yangu. Shika amri zangu katika mambo yote.

7 Na, kama aunashika amri zangu na bkuvumilia hadi mwisho utapata cuzima wa milele, kipawa ambacho ni kikuu katika vipawa vyote vya Mungu.

8 Na itakuja kutokea, kwamba kama utamwomba Baba katika jina langu, kwa imani ukiamini, utampokea aRoho Mtakatifu, ambaye hutoa usemi, ili uweze kusimama kama bshahidi wa mambo ambayo cutayasikia na kuyaona, na pia uweze kutangaza toba kwa kizazi hiki.

9 Tazama, Mimi ni aYesu Kristo, bMwana wa cMungu aliye hai, ambaye daliumba mbingu na edunia, fnuru ambayo haiwezi kufichika ggizani;

10 Kwa hiyo, ni lazima niulete mbele autimilifu wa injili yangu kuanzia kwa bWayunani hadi nyumba ya Israeli.

11 Na tazama, wewe ni David, na wewe umeitwa kusaidia; kitu ambacho kama utakifanya, na ukiwa mwaminifu, utabarikiwa vyote kiroho na kimwili, na kubwa itakuwa thawabu yako. Amina.