Msaada wa Masomo
Wayunani
iliyopita inayofuata

Wayunani

Kama ilivyotumika katika maandiko, Wayunani lina maana kadhaa. Wakati mwingine lina maana ya watu wasiokuwa wa ukoo wa Israeli, wakati mwingine watu wasiokuwa wa ukoo wa Kiyahudi, na wakati mwingine ni mataifa ambayo hayana injili, ingawa panaweza pakawa na watu wa damu ya Kiisraeli miongoni mwa watu hao. Matumizi ya hili la mwisho yanaonekana kutumika zaidi katika Kitabu cha Mormoni na Mafundisho na Maagano.